March 31, 2021

 


Mahakama Kuu Divisheni ya Uhujumu Uchumi maarufu kama Mahakama ya Mafisadi, Dar es Salaam leo Machi 31, 2021 imewahukumu kifungo cha maisha jela mfanyabiashara Abdul Nsembo (45) na mke wake Shamimu Mwasha (41) baada ya kutiwa hatiani kwa makosa ya kujihusisha na dawa za Kulevya aina ya Heroin.

 

Pia mahakama hiyo imetoa amri ya kutaifisha mali za Wahukumiwa ikiwemo gari aina ya Discover 4 ili liwe mali za Serikali, huku dawa hizo zikitakiwa kuteketezwa.

 

Hukumu ya kesi hiyo namba 4 ya mwaka 2020, imetolewa Jaji Elinaza Luvanda baada ya kusikiliza hoja za pande zote mbili kati ya Jamhuri na Utetezi na kujiridhisha kwamba Watuhumiwa wamekutwa na hatiani katika makosa mawili ya usafirishaji dawa za Kulevya.

 

Wawili hao walishtakiwa baada ya kudaiwa Mei Mosi, 2019 wakiwa eneo la Mbezi Beach, Wilaya ya Kinondoni, jijini DSM kinyume na sheria ya uhujumu uchumi walikutwa na dawa hizo.

3 COMMENTS:

  1. Sawa kabisa hawa watu wameshatekeza maisha ya vijana wengi tu wakitanzania hata hii adhabu ni ndogo wangenyongwa hadharani.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Duh!!!
      Mahakama imeshatoa adhabu yake nawe ninani ambae ungetamani watu Hawa wanyongwe?je wewe ni mshauli wa mahakama acha ushabiki kama huo ashumu angekuwa ni ndugu yako je ungethubutu kuongea hayo?

      Delete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic