KAZI inaonekana kuwa nzito kwa kipa namba moja wa Klabu ya Ihefu FC, Deogratius Munish, ‘Dida’ kwenye kulinda ngome yake kwa kuwa amekuwa akitunguliwa kwenye mechi zake uwanjani.
Akiwa ni ingizo jipya dirisha dogo la Januari akiwa ni mchezaji
huru amekaa langoni kwenye jumla ya mechi 9 na ameokota nyavuni jumla ya mabao
15.
Timu yake jumla imeruhusu mabao 34 baada ya kucheza mechi 24
hivyo inaonesha kuwa safu ya ulinzi ya Ihefu inayonolewa na Kocha Mkuu, Zuber
Katwila bado haijawa kwenye ubora.
Kwenye msimamo ipo nafasi ya 17 imekusanya pointi 20 kwa msimu
wa 2020/21.
Katwila amesema kuwa bado wana nafasi ya kufanya vizuri kwenye
mechi zilizobaki.
"Bado kuna mechi ambazo zipo hizo tutazitumia kwa ajili ya kuendelea kupata matokeo chanya hivyo mashabiki watupe sapoti," .







0 COMMENTS:
Post a Comment