March 25, 2021


JERRY Muro, Mkuu wa Wilaya ya Arumeru, mkoani Arusha na Ofisa Habari wa zamani wa Klabu ya Yanga amesema kuwa hajui kama anaweza kubaki kwenye mkoa huo ama anaweza kurejea ndani ya kikosi cha Yanga.


Maneno hayo ameyasema kutokana na aliyempa dhamana ya kuwa kiongozi, kutangulia mbele za haki ambaye ni Rais wa awamu ya tano John Pombe Magufuli na sasa Rais ni Samiah Suluhu.


Muro hivi karibuni amesema:-"Sijui narudi Yanga au naenda wapi maana siwezi kujua huenda ambaye alikuwa ananipenda ni yeye mwenyewe.

"Na mnajua kwamba yule baba alikuwa ni Msukuma na mimi ni Mmachame, lazima niseme ukweli na unajua kwamba kutoboa kwenye ule utawala inahitaji uwezo wa Mungu, kati ya Wamachame wachache nami nilikuwa nipo kwenye utawala wake.

"Nilipata bahati ya kufanya kazi na mheshimiwa Rais, akanipa mkoa mkubwa kuliko yote Tanzania, alinipenda alinitunza," amesema.


Leo Machi 25, mwili wa Magufuli upo Chato ambapo familia itatoa heshima za mwisho na kesho atapumzika katika makazi yake ya milele.


4 COMMENTS:

  1. Sometimes tuwe tunatafakari na kuchagua maneno ya kuongea ambayo yanafika kwenye jamii

    ReplyDelete
  2. ELIMU YA MJINGA HII, NA CV ULIYONAYO BADO UNATAKA KUWA RC TU MILELE?

    ReplyDelete
  3. mbona kazi zipo nyingi tu
    hata kilimo cha mbogamboga kinalipa

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic