March 23, 2021


IMEELEZWA kuwa mabosi wa Yanga wameweka kando mchakato wa kumsaka kocha mpya ambaye atakuja kurithi mikoba ya Cedric Kaze kutokana na msiba wa aliyekuwa  Rais wa Tanzania, John Magufuli katika awamu ya tano.

Kaze alifutwa kazi ndani ya kikosi cha Yanga, Machi 7 kwa kile ambacho kilielezwa kuwa mwendo mbovu wa timu hiyo ambayo inaongoza ligi msimu huu wa 2020/21.

Mechi ya mwisho kwa Kaze kukaa kwenye benchi ilikuwa ni mbele ya Polisi Tanzania na ubao ulisoma Polisi Tanzania 1-1 Yanga, Uwanja wa Sheikh Amri Abeid.

Uongozi wa Yanga kupitia kwa Mwenyekiti wa timu hiyo Mshindo Msolla uliweka wazi kuwa mchakato wa kumsaka mrithi mpya unaendelea na utazingatia vigezo ambavyo vinahitajika.

Habari kutoka ndani ya Yanga imeeleza kuwa mchakato huo umesimamishwa kwa muda mpaka pale hali itakapotulia.

"Kwa sasa mchakato umesimamishwa kumtafuta kocha mpya kutokana na msiba wa Magufuli, baada ya hapo tutajua kwamba nini kitaendelea," .

Makamu Mwenyekiti wa Yanga, Fredrick Mwakalebela amesema kuwa kwa sasa hakuna kocha ambaye anaweza kuja.


"Kwa sasa hakuna kocha ambaye anaweza kuja ndani ya siku hizi tatu kwani tumesimamisha vikao vyote ili kupisha huu msiba wa kitaifa," .

Chanzo Spoti Xtra.

1 COMMENTS:

  1. Mbona mnatuchanganya. Mara keshafika Mfaransa mara atafika kesho mara leo hivi na kesho hili. Lipi tukamate tulikamate

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic