UONGOZI wa Simba, umelazimika kuachana na mshambuliaji wao raia wa Nigeria, Lokosa Junior, baada ya kutoweka kwa siku tatu kwenye mazoezi ya timu hiyo.
Lokosa alijiunga na Simba miezi miwili iliyopita akitokea timu ya Esperance ya Tunisia, aliyokuwa akiitumikia kabla ya kurejea kwao Nigeria ambapo alikuwa nje ya dimba kwa zaidi ya miezi nane.
Simba walimsajili mshambuliaji huyo wakiamini angeweza kurejea kwenye kiwango chake na kuwasaidia katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika hatua ya makundi.
Chanzo chetu kutoka ndani ya Simba, kimeliambia Championi Jumatano kuwa, tayari mabosi wa Simba wamevunja mkataba kimyakimya na nyota huyo, jambo lililomfanya ajiondoe rasmi kwenye mazoezi ya timu hiyo akisubiria maslahi yake ya kuvunjwa kwa mkataba huo ili arejee kwao kujipanga na timu nyingine.
“Nimeamini kweli kwenye mpira mchezaji kama akikaa nje ya uwanja kwa muda mrefu, rekodi yake pekee haiwezi kumlinda, maana juzi nilimsikia mazoezini kocha wetu, Gomes (Didier) akimuulizia Lokosa kwa meneja wa timu ambapo alijibiwa kuwa hajafika mazoezini kutokana na kuwa na mazungumzo na mabosi wetu, lakini ukifuatilia mazungumzo nje ya hapo utaona wazi kuwa hatarudi Simba tena.
"Hadi muda huu ninapoongea na wewe ninauhakika kabisa tayari kakatwa kwenye kikosi na yupo njiani kusepa kwao maana ameshindwa kukidhi mahitaji ya timu na vilevile anaonekana kuwa na majeraha sugu yanayomfanya kuwa muoga kugongana hata mazoezini jambo lililomfanya kocha kutompa nafasi ya kucheza,” kilisema chanzo hicho.
Lokosa tangu ajiunge na Simba alicheza mechi moja akitokea benchi dhidi ya TP Mazembe kwenye michuano ya Simba Super Cup.







Matumizi mabaya ya fedha tutawatumbua
ReplyDeleteFedha zako au? Kiasi gani ushachangia mpk sasa katika sajili za simba?
ReplyDeleteUjinga hauna mpaka.Umechangia shillingi ngapi? Huna hata ya vocha! Wakati mwingine ficha ujuha wako.
ReplyDeleteTatizo hilo
ReplyDeletehalafu ndo nyie kila mkiamka mnamponda sarpong, maisha yana kasi haya hatar
ReplyDeleteHivi sarpong ni mchezaji wa timu gani
ReplyDeleteutamjuaje wakati wewe ni shabiki maandazi.....hata ukiambiwa utaje first eleven ya timu yako huwezi.
Deletehapo ndipo munapo chochola kuweni wapenzi musiwe washabiki
DeleteApo kwa kuwa ni mchezaji wa SIMBA wachawazi maandazi huwasikii kwakua wanapewa posho lkn iwe yanga midomo mpaka ingechanika kwakulizungumzia
ReplyDeletewangapi wapo yanga hawana mchango au nao mulichangia kikubwa pambaneni na hali zenu tyuuu c kujiona waongeaji
ReplyDelete