Raia huyo wa Burundi alikuwa nje ya uwanja kwa muda mrefu akitibu majeraha aliyopata kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Tanzania Prisons na alijitonesha alipocheza fainali ya Kombe la Mapinduzi mbele ya Simba.
Ntibanzokiza alikuwa ni chaguo namba moja la Kocha Mkuu, Cedric Kaze ambaye alifutwa kazi Machi 7 kutokana na kile kilichoelezwa kuwa matokeo mabovu ndani ya kikosi hicho.
Anatarajiwa kuja Bongo Machi 26 Burundi ambapo timu ya Burundi itakuja Tanzania kucheza mchezo wao dhidi ya Afrika ya Kati kwa ajili ya kufuzu Afcon.
Serikali ya Tanzania imeiruhusu Burundi kutumia uwanja wa Benjamin Mkapa katika mchezo huo ambao unatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa.








Kwa nini burundi waje wachezee hapa
ReplyDeletekama unajua kwanini wale waarabu walikuja kucheza na mamelodi hapa basi bila shaka utafahamu kwa nini burundi nao wanakuja hapa.
ReplyDelete