March 2, 2021


 DIDIER Gomes, Kocha Mkuu wa Simba amesema kuwa wapo tayari kwa ajili ya mchezo wao wa Ligi ya Mabingwa dhidi ya Al Merrikh ya Sudan.

Mchezo huo unatarajiwa kuchezwa Machi 6 utakuwa ni wa tatu kwa Simba ndani ya kundi A ambapo inaongoza ikiwa na pointi sita.

Kikosi kinatarajiwa kuanza safari leo kuibukia nchini Sudan ili kujiweka sawa kwa ajili ya mchezo huo huku habari zikieleza kuwa tayari mabingwa hao watetezi wameshawatuma watu wao mapema nchini Sudan.

"Tayari wapo waliotangulia nchini Sudan kwa ajili ya kuweka mazingira sawa. Ipo wazi kwamba maandalizi ya mpira huwa yanaanza mapema hilo ndilo ambalo linafanyika pia ndani ya Simba," .

Baada ya kumaliza mchezo wao wa jana kwa ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya JKT Tanzania, Gomes amesema kuwa wapo tayari kwa ajili ya mchezo huo.

Kocha huyo ambaye ameongoza kikosi hicho kwenye jumla ya mechi tisa akiwa na kombe moja kabatini la Simba Super Cup ameweza kuanza vizuri ndani ya kikosi hicho baada ya kuchukua mikoba ya Sven Vandenbroeck.

5 COMMENTS:

  1. Haya bn wenzetu,,,cc utopolo mmmmh

    ReplyDelete
  2. Mashallah yaani sisi wa ze Utopolo tunalalamika tu kila siku mara marefa, huku tff mara bodi ya ligi. Wajemeni hebu mututurumiage wenzenu. Timechanganyikiwa sana. Ila twawaombeni fanyeni vizuri mutupe lift twende na timu nne safari ijayo hatutawaangusa tena.

    ReplyDelete
  3. Tunawaonea wivu. Sisi acha tupambane na hali yetu. Ila kwa uongozi huu wa akina Tumbotumbo sijui kama tutafika mbali.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic