UONGOZI wa Simba umeweka wazi kuwa utapambana kutimiza agizo la
Rais wa awamu ya tano, John Magufuli la kuwataka watwae ubingwa wa Afrika.
Agizo hilo alilitoa msimu wa 201//18 wakati akiwakabidhi ubingwa
wa Ligi Kuu Bara na alishuhudia timu hiyo ikitunguliwa bao 1-0 dhidi ya Kagera
Sugar.
Magufuli ambaye alitangazwa kufikwa na umauti Machi 17 na Makamu
wa Rais, Samia Suluhu ambaye kwa sasa ni Rais wa awamu ya sita aliweka wazi kwa
kuwaambia Simba anahitaji kuona wakimuita akiwakabidhi Kombe la Afrika jambo
ambalo halijatimia mpaka anafikwa na umauti.
Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara amesema:”Rais wetu ameondoka ghafla na sisi Wanasimba tupo kwenye mashindano ya Ligi ya Mabingwa Afrika na tutashiriki kwa nguvu kubwa na ari ili kuenzi changamoto ambayo alituachia.
" Tukiwa ni Wanasimba, wanasoka agizo lake linapaswa lituongoze ili hatimaye
tufanikiwe kubeba taji la ubingwa wa Afrika,” .
Kwa sasa Simba inayonolewa na Kocha Mkuu, Didier Gomes imetinga
hatua ya makundi inaongoza kundi A ikiwa na pointi 10.
0 COMMENTS:
Post a Comment