March 1, 2021


 DIDIER Gomes, Kocha Mkuu wa Simba amesema kuwa anatambua mchezo wa leo dhidi ya JKT Tanzania utakuwa na ushindani mkubwa ila amewaambia wachezaji wake wanapaswa kupambana ili kupata pointi tatu.

Mchezo wa kwanza uliochezwa Uwanja wa Jamhuri, Dodoma, ubao ulisoma JKT Tanzania 0-4 Simba baada ya dakika 90.

Huku bao la kwanza la Luis Miquissone akiwa nje ya 18 likiwa ni moja ya bao bora na kushangilia kwa kuwafuata mashabiki kulimponza nyota huyo ambapo alionyeshwa kadi ya njano.

Gomes amesema:"Utakuwa mchezo mgumu ila tunahitaji pointi tatu muhimu,ushindi wetu ni mwanzo wa kuendelea kupunguza pointi ambazo tunadaiwa na wapinzani wetu.

"Ukweli ni kwamba kila timu ambayo tunakutana nayo ndani ya uwanja inafanya vizuri katika kusaka matokeo hivyo nasi kazi yetu ni kusaka ushindi,".

JKT Tanzania kwenye msimamo ipo nafasi ya 10 ina pointi 24 baada ya kucheza mechi 21 inakutana na Simba iliyo nafasi ya pili na pointi zake ni 42.


6 COMMENTS:

  1. Mungu Mkubwa na muweza. Hizo point 3 zitapatikana kama zivopatikana hapo awali

    ReplyDelete
  2. Wajipange simba wakiingia na kiburi cha ukubwa wataangukia pua.Ifahamike tu ligi ilipo ni fitna zaidi kuliko mpira uwanjani na JKT anaweza kujazwa upepo tu ili afanye kazi ya Utopolo.Tuliona mara kadhaa wachezaji wa timu za majeshi wakuwafanyia faulo za kijinga wachezaji wa simba lakini kama marefa wakionekana kuchukulia poa.

    ReplyDelete
  3. WANASEMA SIMBA HUA HAWALALAMIKI LAKINI NAONA HAA KABLA MECH HAIJACHEZWA MNAWEZA LAWAMA

    ReplyDelete
    Replies
    1. Jifunze kutofautisha kati ya kulalamika na kutoa angalizo

      Delete
  4. Haitotokea cmb ifanane na utopolo

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic