March 1, 2021


 CEDRIC Kaze, Kocha Mkuu wa Yanga amesema kuwa mpango mkubwa kwa sasa ni kupata matokeo chanya kwenye mechi yao mbele ya Coastal Union.

Yanga ikiwa ni namba moja kwenye msimamo na pointi zake 49 ina kibarua cha kusaka pointi tatu mbele ya Coastal Union Machi 4, Uwanja wa Mkwakwani, Tanga.

Kaze amesema kuwa wachezaji wake wapo vizuri na anaamini kwamba atapata matokeo chanya kwenye mchezo huo.

"Kwa sasa tunatazama namna gani tunaweza kupata matokeo chanya kwenye mechi zijazo ndani ya Uwanja hilo ni la msingi kwetu.

"Kila kitu kitakuwa sawa mashabiki waendelee kutupa sapoti kwa kuwa ushindani ni mkubwa nasi pia tunaendelea kushindana,". 

3 COMMENTS:

  1. Vipi tatizo la kutokujiamini kwa wachezaji wako limeisha??

    ReplyDelete
  2. Kaze ameshindwa kuwanoa washambuliaji wake,hili ni tatizo kubwa na mtajua muda si mrefu

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic