March 18, 2021


 TANZIA

RAIS wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,  John Pombe Magufuli amefariki dunia.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania , Samia Suluhu ametangaza msiba wa Rais, John Pombe Magufuli.


Samia usiku wa kuamkia leo kupitia television ya Taifa ya Tanzania,  TBC amesema kuwa umauti umemkuta Magufuli alipokuwa akipatiwa matibabu.


Ameongeza kwa kusema kuwa Magufuli ametangulia mbele za haki kutokana na tatizo la moyo alilokuwa nalo  muda mrefu.


Utaratibu wa kumpumzisha Magufuli utatolewa na Serikali ambapo kutakuwa na maombolezo ya siku 14 na bendera zitakuwa nusu mlingoti.

Magufuli atakumbukwa kwa mchango wake mkubwa kwa Tanzania na jitihada zake katika kila sekta ikiwa ni pamoja na michezo. 


Pumzika kwa Amani

5 COMMENTS:

  1. Tutazidi kumkumbuka raisi wetu alichokifanya pia, alikua na mchango mkubwa kwa watanzania mungu amlaze mahara pema peponi na apumzike kwa amani (AMINA)

    ReplyDelete
  2. Mbuyu umeanguka....RIP mtetezi wa wanyonge na taifa kwa ujumla.....tutakukumbuka daima katika harakati zako za kulikomboa taifa la tanzania kutoka katika umaskini ambazo kwa bahati mbaya mungu amekuchukua ukiwa bado hujazikamilisha.

    ReplyDelete
  3. Mungu amlaze mahali pema peponi Aliweza kutusaidia wengi Mbele yako nyuma yetu

    ReplyDelete
  4. R.I.P Hayati magufuri tulikupenda ila mungu kakupenda zaidi

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic