March 17, 2021


SAFU ya ulinzi ya Klabu ya Simba inayonolewa na Kocha Mkuu, Didier Gomes imeweza kuweka rekodi ya kuwa ni namba moja kwa kuruhusu mabao machache.

Simba imefungwa mabao 9 ambayo ni machache kwa timu zilizo ndani ya tatu bora, ipo nafasi ya pili, Yanga ipo nafasi ya kwanza, ukuta wake unashika namba mbili kwa kuokota mabao mengi ambayo ni 14.

Ukuta wa Simba unaongozwa na Joash Onyango pamoja na Pascal Wawa ambao wamekuwa na maelewano makubwa na ni chaguo la kwanza kwa Gomes.

Ukuta wa Yanga ulianza kuwa na maelewano mwanzo wa msimu ila kwa sasa taratibu uimara umeanza kumeguka chini ya Lamine Moro na Bakari Mwamnyeto.


Azam FC iliyo nafasi ya tatu ukuta wake ni namba tatu kwa kuokota mabao mengi ikiwa imeruhusu mabao 17 katika mechi 24 msimu wa 2020/21. Kiongozi wake ni Yakub Mohamed.

 

 

5 COMMENTS:

  1. Mwandishi unazi wa Utopolo umekujaa kiasi unashindwa kuandika ukweli. Kwa kuwa roho inakuuma, unajikuta unajiumauma mara ukuta wa Simba unashika namba 2 kwa kuruhusu magoli 9; kisha ukuta wa Yanga unashika namba moja kwa kuruhusu magoli 14. Aibu hii....

    ReplyDelete
  2. Mapenzi yako dhidi ya yanga mpaka unapotosha ukweli hivi aliyefungwa mabao 14 anampitaje aliyefungwa mabao 9

    ReplyDelete
    Replies
    1. Katumia lugha ya wapiga debe, “biguruni mia mbili posta gari” 😂😂😂

      Delete
  3. najaribu elewa ulichoandika
    Yanga imeshika nasafi ya kwanza ila ukuta wake ni namba mbili umeokota mabao 14.
    Azam imeruhusu 17 hivyo inamaanisha imeokota bao 17 na ikawa ya pili..
    Mwandishi utopolo...kufuatana na ulivyoandika 17 na 14 ni ipi kubwa? na kama simba imeokota bao 9 inakuwaje iwe ya pili kati ya timu zilizookota bao 14 na 17.. hujui hesabu kabisa na pia hujui kuandika. huwezi changanya vitu.. kama ni msimamo wa ligi kufuatana na pointi 1. Yanga, 2 Simba 3 Azam..Kama ni kuruhusu magoli 1. Azam 2 Yanga, 3 Simba.,Sio unaandika andika tu rudi shule..Je na kichwa cha habari? halisia ni kuwa Simba imewaacha na sio inakimbiza

    ReplyDelete
  4. Ila kuelewa ni kazi someni vizur mtaelewa alichoandika

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic