April 4, 2021

BAADA ya kukamilisha usajili wa kujiunga na kikosi cha Nkana kwa mkataba wa mwaka mmoja, mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania, Eliud Ambokile amesema kuwa ana mategemeo makubwa ya kufanya vizuri akiwa nchini Zambia.

Tangu ajiunge na TP Mazembe mwezi Juni, 2019 Ambokile amekuwa na wakati mgumu kupata nafasi ndani ya kikosi cha kwanza ambapo kwa msimu huu pekee hajacheza mchezo wowote kwenye Ligi Kuu ya DR Congo.

Akizungumzia mipango yake baada ya kukamilisha usajili huo, Ambokile amesema: “Ni kweli nashukuru Mungu kwa kukamilisha usajili wangu wa kujiunga na klabu ya Nkana ya Zambia kutokea Mazembe.

“Nkana wamenisajili kama mchezaji huru na tayari nimesaini mkataba wa mwaka mmoja, ni matumani yangu baada ya kukosa nafasi ya kucheza nikiwa na Mazembe, nitapata nafasi ya kuonyesha uwezo wangu ndani ya kikosi cha Nkana,”

1 COMMENTS:

  1. Hiyo ndo njia ya kurudi kwenye timu yake bongo tpe muda mfupi tutamuona huku

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic