April 20, 2021


 SELEMAN Matola, Kocha Msaidizi wa Simba amesema kuwa wanatambua kwamba wapinzani wao Kagera Sugar ni wazuri wakiwa Uwanja wa Kaitaba jambo ambalo linawafanya wajipange kuingia kwa tahadhari.

Kesho, saa 10:00 usiku kutakuwa na mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Kagera Sugar ambao utachezwa Buoba.

Katika mchezo wa kwanza walipokutana Uwanja wa Uhuru, Simba ilishinda mabao 2-0 jambo lililowafanya wasepe na pointi tatu kwenye mchezo huo uliokuwa na ushindani mkubwa.

Simba inapambana kutetea taji la ligi ikiwa namba mbili na pointi zake kibindoni ni 52 baada ya kucheza mechi 22 huku Kagera Sugar imejichimbia nafasi ya 14na pointi 27.

Matola amesema:"Tunatambua kwamba Kagera Sugar ni timu imara ikiwa Uwanja wa Kaitaba hivyo tutaigia kwenye mchezo huo tukiwa tunajua kwamba tunakutana na timu bora.

"Kuanzia kwa wachezaji wote wapo tayari kwa ajili ya mchezo wa kesho na wataanza kwa ari kubwa ili kupata matokeo chanya katika mchezo huo," amesema.

5 COMMENTS:

  1. Mwandishi uwe una edit makala kabla haijatoka rasmi,usidharirishe journalist,umeandika saa kumi usiku badala ya saa kumi jioni.Nimefatilia makala zako nyingi huwa unakosea Sana.

    ReplyDelete
  2. Mechi inachezwa saa kumi udiku? Ha ha ha, uwe makini bwana mwandishi

    ReplyDelete
    Replies
    1. mbona na wewe umeandika saa kumi udiku badala ya usiku?

      Delete
  3. Niliona ni jambo geni sana. Makala kabla ya kutolewa rasmi ni lazima yarejewe kwanza.Nikahisi kuwa hao hawendi kucheza mpira bali kula dsku

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic