April 9, 2021


 IKIWA leo Aprili 9, Azam FC inakutana na Mtibwa Sugar kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara mzunguko wa pili rekodi zinaonyesha kuwa Azam FC, imekutana mara 25 na Mtibwa Sugar kwenye mechi za Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL).


Azam FC imeshinda mechi 11 mbele ya Mtibwa Sugar zimepatikana sare tisa huku Mtibwa Sugar ikishinda mechi tano.

Mechi tano ilizopoteza Azam FC, nne imefungwa ugenini mkoani Morogoro na moja kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam, ikiwa haijawahi kupoteza katika dimba lake la Azam Complex.

Jumla ya mabao 49 yamefungwa kwenye mechi hizo, Azam FC ikiwa imefunga mabao 31 huku ikiruhusu nyavu zake kutikiswa na Mtibwa mara 18.


Mzunguko wa kwanza walipokutana Uwanja wa Jamhuri, Moro ubao ulisomwa Mtibwa Sugar 1-0 Azam FC.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic