HAKUNA kulala! Ndivyo utakavyosema mara baada ya kutua Cairo, Misri kikosi cha Simba kilifanya mazoezi kwa saa mbili katika kujiandaa na mchezo wao dhidi ya Al Ahly.Yote hayo ni katika kujiandaa na mchezo huo wa leo Ijumaa wa Ligi ya Mabingwa Afrika utakaopigwa saa nne kamili usiku.
Timu hizo zote tayari zimefuzu hatua inayofuata, Simba wakiwa kileleni katika Kundi A kwa kuwa na pointi 13 wakati Al Ahly wanashika nafasi ya pili kwa kuwa na pointi 8.
Kwa mujibu wa taarifa ambazo imezipata Championi Ijumaa, kutoka ndani ya benchi la ufundi la timu hiyo linaloongozwa na Mfaransa, Didier Gomes, timu hiyo mara baada ya kutua Misri, ilifanya mazoezi kwa saa mbili kuanzia saa tatu hadi tano usiku ndipo waliporejea hotelini kupumzika.
Aliongeza kuwa timu hiyo tangu wamefika huko wamekuwa wakipata sapoti kutoka kwa wapinzani wa Al Ahly ambao ni Zamalek kwa kuwapa mbinu na fitina ambazo wanazozitumia katika kuhakikisha wanapata ushindi katika mchezo huo.
“Tulifahamu hilo la fitina kuwepo, kwani wenyeji wetu wametangaza mabadiliko ya uwanja utakaotumika katika mchezo huo wa mwisho.
“Al Ahly katika michezo iliyopita dhidi ya Al Merrikh na AS Vita walitumia Uwanja wa Kimataifa wa Cairo, lakini katika mchezo wetu huu utachezwa kwenye Uwanja wa Al-Salam WE ambao unamilikiwa na Al Ahly wenyewe.
“Uwanja wa Kimataifa wa Cairo, unaingiza mashabiki 100,000 wakati ule wa Al-Salam WE unaingiza mashabiki 30,000 lakini hiyo haiwezi kutufanya tutoke mchezoni na badala yake tutajipanga kupata matokeo mazuri,” alisema bosi huyo.
Katika hatua nyingine, Mtendaji Mkuu (C.E.O) wa Simba Barbara Gonzalez, leo (jana) usiku alitarajiwa kufanya kikao cha pamoja na wachezaji, benchi la ufundi katika kuwaongezea morali ya kujituma.
Kikao hicho kilitarajiwa kufanyika katika hoteli hiyo waliyofikia mara baada ya kumaliza mazoezi ya timu hiyo kabla ya leo kuingia uwanjani kuvaana na Al Ahly.
Kwani kanuni za CAF kuhusu hilo zinasemaje, ninachojua ni kuwa kabla ya mashindano kuanza kila timu inasema itatumia gani
ReplyDelete