KIUNGO wa klabu ya soka ya KMC, Abdallah Masoud ‘Cabaye’ amefunguka kuwa alilazimika kumfanyia madhambi kiungo wa Yanga, Saidi Ntibazonkiza ‘Saido’ na kupewa kadi nyekundu kwa kuwa hiyo ndiyo njia pekee ambayo ingeweza kumzuia Saido asifunge bao la ushindi kwa Yanga
Cabaye alionyeshwa kadi hiyo dakika ya 90 ya mchezo baada ya kumfanyia madhambi Saido aliyekuwa katika nafasi nzuri ya kufunga bao nje kidogo ya eneo la 18.
Mchezo huo ulimalizika kwa sare ya bao 1-1 na kuwafanya KMC kufikisha pointi 36, zinazowaweka katika nafasi ya sita ya msimamo baada ya kucheza michezo 25.
Akizungumzia maamuzi hayo, Cabaye amesema: “Kwanza ni jambo la kushukuru kuona wote tumemaliza mchezo salama, kama KMC tulijipanga vizuri kuhakikisha tunapata pointi tatu muhimu katika mchezo, lakini hatukufanikiwa.
“Kuhusiana na kadi nyekundu
niliyoipata, ilikuwa ni kadi halali kwani nilimfanyia madhambi Saido, ambaye
alikuwa kwenye nafasi nzuri ya kutufunga bao tena dakika za mwisho, hivyo
nilifanya vile kwa ajili ya kuiokoa timu yangu,”
0 COMMENTS:
Post a Comment