April 13, 2021

MSHAMBULIAJI wa klabu ya Simba anayehudumu kwa mkopo katika kikosi cha KMC, Charles Ilanfya amesema, washambuliaji wa klabu ya Yanga ni wazuri, lakini changamoto yao kubwa ni kwamba wanakosa utulivu.

Jumamosi iliyopita Ilanfya alikuwa sehemu ya kikosi cha kwanza kilichoanza na kuisumbua sana safu ya ulinzi ya Yanga, katika mchezo wa Ligi Kuu Bara uliopigwa kwenye uwanja wa Mkapa, Dar es Salaam na kumalizika kwa sare ya bao 1-1.

Ilanfya ambaye yupo kwa mkopo wa miezi sita ndani ya KMC akitokea Simba, mpaka sasa amefanikiwa kuifungia KMC mabao mawili kwenye Ligi Kuu Bara.

Akizungumzia safu ya ushambuliaji ya Yanga Ilanfya amesema: “Mchezo wetu wa Jumamosi dhidi ya Yanga ulikuwa mgumu kutokana na ubora wa wapinzani wetu, lakini jambo zuri ni kwamba tulipambana na tunashukuru kwa matokeo ya pointi moja ambayo tuliipata baada ya kupata sare.

“Naweza kusema Yanga walifanikiwa kutengeneza nafasi nyingi za kufunga mabao lakini washambuliaji wao hawakuwa na utulivu na kupelekea kupoteza nafasi hizo, lakini hata sisi tulipata nafasi na hatukuzitumia hivyo ni sehemu ya mpira unapokosea unapata nafasi ya kujifunza,”

 

 


5 COMMENTS:

  1. Wewe uliyekosa goli na nyavu una utulivu kiasi gani kazi kuongea pumba

    ReplyDelete
  2. Pale Simba Sven baadaye alimtoa kbs katika mipango yake, ikidaiwa kuwa kila kocha huyo alipokuwa anampa maelekezo, alishindwa kuyafuata.

    ReplyDelete
  3. Mchezaji afundishwe namna ya kujibu maswali ya waandishi wa habari

    ReplyDelete
  4. Tatizo utopolo hamtakagi kuambiwa ukweli na ndio Maana mmewasomea ALBADIRI waandishi wa habari halafu ni wabishi kweli Yani akili zenu zinafanana,hata kama Ilanfya amekosa magoli lkn anaawambia ukweli kwamba wachezaji wenu hawana utulivu

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic