April 13, 2021


 


ILI kurudisha makali ya kikosi chake, Kaimu kocha Mkuu wa klabu ya Yanga, Juma Mwambusi amesema kuwa anatarajia kufanya mabadiliko makubwa kwenye baadhi ya nafasi za kikosi chake ikiwemo safu za ulinzi na ushambuliaji.

Yanga Jumamosi iliyopita iliandikisha mchezo wa tatu mfululizo bila ushindi baada ya kutoa sare ya bao 1-1 dhidi ya KMC, katika mchezo uliopigwa kwenye uwanja wa Mkapa jijini Dar es Salaam.

Akizungumzia mipango yake, Mwambusi amesema: “Baada ya kupata sare na KMC katika mchezo wetu uliopita, kikosi chetu sasa kinaendelea na mazoezi kujiandaa na mchezo ujao dhidi ya Biashara United, tunajua tunapaswa kufanya vizuri katika mchezo huo ili tupate ushindi na kurejesha hali ya kujiamini na ushindani.

“Kuelekea mchezo huo dhidi ya Biashara tutaendelea kuona mabadiliko katika nafasi kadhaa ndani ya uwanja, ikiwemo kwenye safu ya ushambuliaji na ulinzi kama ambavyo tuliona dhidi ya KMC ambapo Abdallah Shaibu ‘Ninja’ alianza.

“Tunafanya hivi ili kuona tunapata uwiano mzuri wa matumizi ya wachezaji wetu na kupunguza makosa yetu, ili kuhakikisha tunamaliza kiu ya mashabiki wetu ya kukosa ushindi kwa muda mrefu,”

2 COMMENTS:

  1. Biashara kacheza ijumaa halafu anacheza na coastal kabla ya kucheza na yanga ambayo imepewa mapumziko wiki nzima baada ya kucheza na kmc halafu mnatoka kulalamika bodi na tff zinawahujumu

    ReplyDelete
  2. Mwambusi acha kuchonga. Hao wachezaji wa yanga ni vimeo, hata upangue namna gani saizi yenu ni sare au kufungwa. Bado azam atawalambisha ukoka ndiyo mpate adabu

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic