April 9, 2021

 

WAKIWA wanajiandaa na mchezo wao wa leo wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya klabu ya Al Ahly, Uongozi wa klabu ya Simba umelazimika kuwaongeza ulinzi nyota wa kikosi chao hasa Luis Miquissone na Clatous Chama ambao wameonekana kusakwa tangu kikosi chao kilipotua.

Taarifa za kuaminika kutoka chanzo cha karibu cha Simba kimetutonya kuwa tangu walipotua kwenye uwanja wa ndege wa Cairo juzi Jumatano, wakazi wengi wa jiji la Cairo wamekuwa wakitafuta nafasi ya kuwaona wachezaji wa Simba huku Luis na Chama wakionekana kuuliziwa zaidi.

Nyota hao wawili wiki iliyopita walichaguliwa kuingia ndani ya kikosi bora cha Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya kuhusika katika mabao yote manne waliyoyapata katika ushindi wa mabao 4-1 dhidi ya AS VIta, ambapo Chama pia alichaguliwa kuwa mchezaji bora wa wiki wa michuano hiyo.


2 COMMENTS:

  1. Wanawasaka kuwadhuru, kuwanunua au kuwaona tuu live?

    ReplyDelete
  2. Wanataka kuwabaka mi mwarabu namkubali tangu siku ileee alivyobaka simba 5

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic