"AMEWAKA" ndicho unachoweza kukisema kwa kile kinachoonyeshwa na mshambuliaji wa klabu ya soka ya
Yanga raia wa Burundi, Fiston Abdoul Razak ambaye amefanikiwa kuweka kambani mabao manne katika michezo miwili ya kirafiki waliyocheza hivi
karibuni.
Katika michezo hiyo, kwenye mchezo wa kwanza Fiston akiichezea timu ya wachezaji wa Yanga walioitwa kwenye timu za taifa dhidi ya wale waliobaki kambini alifunga mabao matatu, kabla ya Jumanne jioni kufunga bao moja katika ushindi wa mabao 3-0 walioupata dhidi ya African Lyon.
Tangu akamilishe usajili wake wa kujiunga na kikosi cha Yanga, Fiston amefanikiwa kufunga mabao mawili katika michezo mitano aliyoichezea timu hiyo (Bao moja katika michuano ya kombe la FA huku bao moja akifunga katika mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Polisi Tanzania).
Amewaka mazoezini, tusubiri mechi za mashindano
ReplyDeleteHata mazoezini ilikuwa bado
Delete