KELECHI Iheanacho nyota wa Klabu ya Leicester City amesema kuwa anawashukuru mashabiki kwa sapoti yao na kuahidi kuendelea kupambana kwa ajili ya mafanikio ya timu hiyo.
Usiku wa kuamkia leo, Uwanja wa Wembley, Iheanacho alikuwa shujaa alitupia bao la ushindi dakika ya 55 katika nusu fainali ya Kombe la FA mbele ya Southampton ambayo imefungashiwa virago katika Kombe hilo.
Ushindi huo unaipa nafasi Leicester City kutinga hatua ya fainali na itakutana na Chelsea ambayo iliitoa Manchester City katika hatua ya nusu fainali.
Ikiwa na miaka 137 Leicester City haijawahi kushinda taji la FA licha ya kufika katika fainali zake mara nne ila wana taji la Ligi Kuu England ambalo walilitwaa miaka mitano iliyopita.
Nyota huyo amesema:"Asanteni sana kwa sapoti yenu mashabiki wenu kwa kila mmoja kutoka nyumbani, ninawashukuru kwa mara nyingine tena.
"Nina amini kwamba tutaonana kwenye fainali ila endeleeni kukaa salama huko mlipo," .
0 COMMENTS:
Post a Comment