April 19, 2021


 SALHINA Mjengwa, Kocha Mkuu wa Mwadui FC amesema kuwa laiti kama wachezaji wa Simba wangekuwa upande wake basi ingekuwa rahisi kushinda mchezo wa jana Aprili 18 mbele ya Simba.

Mwadui FC iliyo nafasi ya 18 na pointi 16 ilipoteza mbele ya Simba kwa kufungwa bao 1-0 na kuwafanya waziache pointi sita jumlajumla kwa wapinzani hao msimu huu wa 2020/21.

Mchezo wa kwanza walipokutana Uwanja wa Uhuru ubao ulisoma Simba 5-0 Mwadui na jana pia walipoteza kwa bao la ushindi lililofungwa na nahodha mzawa, John Bocco.

Mjengwa amesema kuwa:"Laiti kama wachezaji wa Simba wangekuwa upande wangu nina amini kwamba nasi tungeshinda ila tumeshindwa kupata matokeo kutokana na uzoefu.

"Wachezaji walikuwa wanatengeneza nafasi ikawa ni ngumu kuzibadili kuwa goli, bado tuna mechi mbele nina amini kwamba makosa tutayafanyia kazi," amesema.

Baada ya Simba kusepa na pointi tatu inafikisha jumla ya pointi 52 ikiwa nafasi ya pili na imecheza mechi 22, kinara ni Yanga mwenye pointi 54 baada ya kucheza mechi 25.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic