April 19, 2021


 HABIB Kondo, Kocha Msaidizi wa KMC, amesema kuwa malengo makubwa ya timu hiyo ndani ya Ligi Kuu Bara ni kumaliza ndani ya tano bora kwa msimu wa 2020/21.

Mchezo wake uliopita, Ijumaa, Kondo alishuhudia vijana wake wakisepa na pointi tatu mbele ya Gwambina FC kwenye mchezo wa ligi uliochezwa Uwanja wa Uhuru.

Ni Charles Ilanfya dakika ya 51 alifunga bao la kwanza, kisha Emmanuel Mvuyekure (dk 62) na msumari wa mwisho ulipachikwa na Ally Ramadhan ‘Oviedo’ dakika ya 72.

Akizungumza na Saleh Jembe, Kondo amesema:“Tupo kwenye msako wa pointi tatu, na sababu kubwa ni kuona kwamba timu inamaliza nafasi tano za juu kwenye msimamo. Bado tunaendelea kupambana.

"Nawapongeza wachezaji kwa kuwa wamekuwa wakifanya vizuri kwenye mazoezi na nina amini kwamba wataendelea kupambana kwa ajili ya mechi zetu zijazo, nafasi ipo na tutafanya vizuri," amesema.

Mchezo ujao wa KMC ni dhidi ya Biashara United ambayo imetoka kupoteza kwa kufungwa bao 1-0 dhidi ya Yanga, utachezwa Uwanja wa Uhuru.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic