April 9, 2021


 


KATIKA kuonyesha kweli wao ni moto wa kuotea mbali msimu huu, kikosi cha klabu ya Simba kimekimbiza kwelikweli kitakwimu katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika hatua ya makundi.

Simba inaifukuzia kwa karibu vigogo wa Afrika na klabu inayohofiwa zaidi kwa sasa, Mamelodi Sundowns kupitia takwimu zao katika michuano hiyo.

Mpaka sasa katika michuano hiyo Simba na Mamelodi ndiyo klabu pekee ambazo hazijapoteza mchezo wowote wakiwa wamecheza michezo mitano, na kushinda michezo minne na kutoa sare moja hivyo kila timu kufikisha pointi 13 mpaka sasa.

Kwenye mabao ya kufunga mpaka sasa, Mamelodi wamefanikiwa kuweka kambani mabao 10 huku Simba wao wakiwa wamefunga mabao tisa hivyo wanazidiwa bao moja pekee.

Kwenye mabao ya kufungwa Simba wameonekana kuwa bora zaidi, ambapo safu yao ya ulinzi mpaka sasa imekubali kufungwa bao moja pekee, huku Mamelodi wao wakikubali kufungwa mabao mawili, hivyo kuzifanya timu zote mbili kuwa tofauti ya mabao nane ya kufunga na kufungwa.

 

 

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic