April 4, 2021


 DIDIER Gomes, Kocha Mkuu wa timu ya Simba amewambia beki wa kati Ibrahim Ame ili aweze kutunishiana misuli na kisiki Joash Onyango pamoja na Pascal Wawa ni lazima apende anachokifanya na kuongeza juhudi mara dufu.

Ame ni ingizo jipya ndani ya kikosi hicho kinachoshiriki Ligi ya Mabingwa Afrika kikiwa kimetinga hatua ya robo fainali na mchezo mmoja mkononi bado kwenye hatua ya makundi. Alijiunga na Simba akitokea Coastal Union ya Tanga.

Amecheza mechi 10 akiwa Simba na kutumia jumla ya dakika 665, ni mechi saba alianza kikosi cha kwanza huku tatu akianzia benchi.

Ilikuwa mbele ya Kagera Sugar dk 90, Coastal Union dk 22, Polisi Tanzania 90,Mbeya City 90 na alionyeshwa kadi ya njano kwenye mchezo huu, Ihefu dk 71 na Azam FC dk 90 hizi zilikuwa ni za ligi.

Majimaji dakika 90 na African Lyon dakika 90 hizi zilikuwa ni Kombe la Shirikisho na alitumia dakika 32 kwenye mechi mbili za Ligi ya Mabingwa Afrika ilikuwa mbele ya Plateau United.

Katika mechi hizo ambazo amecheza ametupia bao moja ilikuwa mbele ya Kombe la Shirikisho dhidi ya Majimaji kwa kichwa akitumia pasi ya Rarry Bwalya.

Gomes amesema kuwa ili Ame aweze kupata namba mbele ya Onyango na Wawa ni lazima ajitume zaidi yao kwa kuwa ushindani ni mkubwa.

 

3 COMMENTS:

  1. Usingojee kesho kwani dakika iliyokwenda haitorejea nyuma tena

    ReplyDelete
  2. Ushauri Mzuri.Ame ana vitu vingi vinavyoweza kumfanya kuwa miongoni mwa beki bora Tatizo ni uzoefu na ili kupata uzoefu lazima acheze.Sio rahisi kuwaweka benchi Wawa na Onyango lakini inawezekana na Kama ataweza basi anaweza kwenda kucheza hata Alahly.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic