April 4, 2021

 


KAIMU Kocha Mkuu wa Klabu ya Yanga, Juma Mwambusi amesema kuwa anaamini washambuliaji wake watawashangaza wengi ligi itakapoanza kutokana na program ambazo wanazifanya.

Akizungumza na Saleh Jembe, Mwambusi amesema kuwa kwa sasa kazi kubwa ambayo wanaifanya ni kuwarejeshea hali ya kujiamini pamoja na uwezo wa kumiliki mpira jambo ambalo naamini litawarudisha katika kasi.

“Ukitazama muda ambao nipo na vijana ninaona mabadiliko kila leo, wataweza kuwa katika kasi ya tofauti ambayo itawashangaza wengi kwa kuwa kila kitu naona kinakwenda sawa.

“Upande wa Fiston, (Abdulazack), Sarpong,(Michael) ni wachezaji wazuri na wote ninakwenda nao sawa hivyo sina mashaka na uwezo wao nina amini kwamba kazi yao ya kufunga wataitimiza ni suala la kusubiri,” amesema.

Yanga itaanza kumenyana na KMC kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara unaotarajiwa kuchezwa Aprili 10, Uwanja wa Mkapa.

Mchezo wao wa mzunguko wa kwanza ubao ulisoma KMC 1-2 Yanga na kuwafanya Yanga wasepe na pointi tatu huku KMC wakikosa pointi hizo Uwanja wa CCM Kirumba hivyo utakuwa mchezo wenye ushindani.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic