April 7, 2021


 ZUBER Katwila, Kocha Mkuu wa Ihefu FC yenye maskani yake Mbeya amesema kuwa wanahitaji pointi tatu muhimu kwenye mchezo wao wa ligi dhidi ya Namungo FC utakaochezwa Uwanja wa Majaliwa.

Ihefu kwenye msimamo ipo nafasi ya 17 ina pointi 20, inakutana na Namungo FC iliyo nafasi ya 10 na pointi zao kibindoni ni 27.

Akizungumza na Saleh Jembe kuelekea kwenye mchezo huo unaotarajiwa kuchezwa Aprili 8, Katwila amesema kuwa wanachohitaji kwenye mchezo huo ni pointi tatu.

“Tupo kwenye nafasi mbaya kwa sasa tunapambana ili tujinasue hapa tulipo, hivyo nimewaambia wachezaji wanapaswa wajiamini na tupambane kupata pointi tatu kwenye mechi zetu.

“Haitakuwa kazi rahisi hasa ukizingatia kwamba mzunguko wa pili kila timu inahitaji pointi tatu. Mashabiki waendelee kutupa sapoti kila kitu kitakuwa sawa,”. 

Kwenye msimao wa ligi, Ihefu FC ipo nafasi ya 17 na pointi 20 inakutana na Namungo FC iliyo nafasi ya 10 na 27.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic