April 7, 2021


 MUSTAPHA Ghorbal, mwamuzi wa kati mwenye beji ya Fifa anatarajiwa kuwa pilato kwenye mchezo wa hatua ya makundi kati ya Al Ahly dhidi ya Simba unaotarajiwa kuchezwa Aprili 9.

Raia huyo wa Algeria ana umri wa miaka 35 ni miongoni mwa wale ambao wanachezesha pia Ligi Kuu ya Algeria.

Rekodi zinaonyesha kuwa alianza kazi hiyo mwaka 2010 na mpaka mwaka 2020  amechezesha jumla ya mechi 115 za ligi ya Algeria akiwa ameonyesha jumla ya kadi 390 za njano na kadi 18 nyekundu.

2020 kwenye mashindano ya Caf alichezesha fainali kati ya Al Ahly dhidi ya Zamalek na ubao ulisoma Al Ahly 2-1 Zamaleck.

Katika mchezo huo wa Ligi ya Mabingwa Afrika hatua ya makundi kati ya Al Ahly v Simba timu zote mbili zimetinga hatua ya robo fainali ambapo kwenye kudni A, Simba ni vinara na wana pointi 13 huku Al Ahly wakiwa na pointi 8.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic