April 24, 2021


 HARRY Kane, nahodha wa kikosi cha Tottenham kuna hatihati kesho akakosekana kwenye mchezo wa fainali ya Carabao Cup dhidi ya Manchester City.

Kane aliumia kifundo cha mguu Ijumaa iliyopita wakati timu yake ilipokuwa ikipambana na Everton mchezo ambao ulikuwa ni wa mwisho kwa Jose Mourinho kabla ya kufutwa mazima.

Nyota huyo mwenye miaka 27 wakati timu yake ikishinda mabao 2-1 dhidi ya Soouthampton ndani ya Ligi Kuu England alikosekana kutokana na maumivu.

Taarifa zimeeleza kuwa Kane ambaye ni namba moja kwa utupiaji katika kikosi hicho ametupia jumla ya mabao 26 katika michuano yote alianza mazoezi na wenzake lakini hali ya kuwa fiti kwa ajili ya mchezo wa kesho bado haijajulikana.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic