April 13, 2021

UONGOZI wa kikosi cha klabu ya KMC, umesema kuwa sababu kubwa ya kushindwa kutoa maelezo kuhusu ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), inayoeleza kuwa klabu hiyo inadaiwa na Manispaa ya Kinondoni ni majukumu waliyokuwa nayo ya kujiandaa na mchezo dhidi ya Yanga.

Katika ripoti hiyo iliyotolewa Alhamisi iliyopita, KMC inadaiwa kuchukua mkopo wa Shilingi Milioni 33 kutoka Manispaa ya kinondoni msimu wa 2019/20 kwa ajili ya malipo ya kocha lakini hawajafanya marejesho.

KMC na Yanga juzi jioni zilikutana katika mchezo wa mzunguko wa pili wa Ligi Kuu Bara, uliopigwa katika uwanja wa Mkapa jijini Dar es Salaam.

Akizungumzia sakata hilo, Ofisa habari wa KMC, Christina Mwagala amesema: “Ni kweli tumeisikia hiyo ripoti ya CAG kuhusu klabu yetu kuchukua mkopo wa kiasi cha fedha kutoka katika uongozi wa Manispaa ya Konondoni.

“Lakini taarifa hii imetufikia ambapo kama taasisi tulikuwa na majukumu mengine ya maandalizi ya mchezo wetu dhidi ya Yanga, hivyo hatujapata nafasi ya kukaa pamoja na kuliangalia suala hilo la CAG.

“Lakini baada ya kumaliza mchezo huo sasa tutakaa, na kama kutakuwa na taarifa yoyote ya maelezo tutaiwasilisha,”

 

1 COMMENTS:

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic