KIUNGO mshambuliaji wa Azam FC, Idd Seleman 'Nado', ameongeza mkataba mpya wa miaka miwili kuendelea kusalia kwenye viunga vya Azam Complex.
Nado amesaini mkataba huo leo Jumanne Aprili 13 mbele ya Ofisa Mtendaji Mkuu, Abdulkarim Amin 'Popat', utakaomfanya aendelee kusalia Azam FC hadi mwaka 2024.
Nyota huyo amekuwa na kiwango tokea msimu uliopita alipojiunga Azam FC akitokea Mbeya City, hadi sasa msimu huu amehusika kwenye mabao 12 ya Azam FC, akifunga mara saba na kutoa pasi za mwisho tano.
Ameshasinya miwili tena
ReplyDelete