Uwanja wa Mkapa
Namungo FC 0-0 Nkana FC
Mapumziko
Zinaongezwa dakika 2
Dakika ya 45 Sabilo anakosa nafasi ya wazi kwa kupiga kichwa kinakwenda nje ya lango
Dakika ya 42 Duah anapeleka mashambulizi Nkana FC
Dakika ya 36, Tangalo Fred anaingia anatoka Nyenye
Dakika ya 34 Nyenye anacheza faulo nje kidogo ya 18 linaokolewa na Nahimana
Dakika ya 33 Kichuya anafanya jaribio linakwenda nje ya lango
Dakika ya 29 wanapata faulo ndani ya 18
Dakika ya 20 mabeki wa Namungo FC wanamsindikiza mshambuliaji wa Nkana FC anapiga shuti linakwenda nje ya lango
Dakika ya 15 Shamte anapeleka mashambulizi Nkana inakuwa ni kona inapigwa na Shiza Kichuya ni kona fupi
Dakika ya 12, Sabilo anaotea
Dakika ya 7 Hamis Nyenye wa Namungo anaonyeshwa kadi ya kwanza ya njano kwenye mchezo wa leo
Dakika ya 5 Stephen Sey wa Namungo anakosa nafasi ya wazi akiwa na mlinda mlango
Dakika ya 2 Nahimana anaokoa hatari langoni mwake
Baada ya vuta nikuvute kati ya Nkana FC na Mwamuzi wa mchezo wa leo hatimaye wamekubaliana kuanza mchezo ulitarajiwa kuanza saa 10:00 ila umeanza saa 11:00
Kulikuwa na dakika moja ya kumuombea aliyekuwa Rais wa awamu ya tano John Pombe Magufuli
Kichwa Cha mbuzi
ReplyDeleteNamungo sasa kwa heri, ajaribu mwakani
ReplyDeleteNamungo walisafiria nyota ya corona kuingia kwrnye makundi hawakukutana upinzani mkali huko mwanzo
ReplyDeleteNamungo walisafiria nyota ya corona kuingia kwrnye makundi hawakukutana upinzani mkali huko mwanzo
ReplyDeleteWakati utopolo wanasema SIMBA amesafiria nyota Corona, ila Namungo yeye alikua anapambana dah hawa jamaa hawajielewi hata kidogo ila mwakan tunawabeba hivyo hivyo, ijapokua wanaongea sana.
ReplyDeleteHalafu mnalalamika ooh simba inawachezaji wengi wa kigeni inaua soka letu ooh blahblah kibao.hao namungo asilimia kubwa ni wazawa angalia wanavyocheza unaona kabisa hawajaiva kwa mashindano makubwa mpira ni biashara kubwa acheni wenye pesa wafanye yao kupitia mpira waingize pesa
ReplyDeleteWakiambulia hata point moja wakatambike
ReplyDelete