April 4, 2021


 KLABU ya Nkana FC ya Zambia imegoma pia kuweza kuingia Uwanja wa Mkapa kwa ajili ya kuanza mchezo wa leo dhidi ya Namungo FC ya Ruangwa.


Awali iligoma kufanya mazoezi katika Uwanja wa Mkapa na ilifanyia nje ya uwanja sehemu ya parking ya magari.


Mchezo wa leo ni wa Kombe la Shirikisho hatua ya makundi na timu zote zipo kundi D na kati ya hizo hakuna hata moja ambay imeweza kushinda mchezo hata mmoja kati ya miwili ambayo imecheza.

Sababu ya Nkana kufanya hivyo ni kile ambacho wanadai kuwa kuna hujuma ambazo wamefanyiwa na wapinzani wao.

Pia wamegoma kufanya vipimo vya Corona kwa maelezo kuwa wamepima nchini Zambia hivyo hawawezi kupima kwenye ardhi ya Tanzania.

Namungo wapo tayari kwa ajili ya mchezo wa leo ambao ni wa tatu kwenye hatua ya makundi ndani ya Kombe la Shirikisho.

1 COMMENTS:

  1. Hawa sasa ni washamba kumbe, wanaogopa hata namungo? Wangekuwa simba jee? Si wasingetia hata mguu nchini. Basi wanapoteza point 3 muhimu

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic