April 4, 2021

 


WAKIWA Uwanja wa Emirates, jana vijana wa Jurgen Klopp wamesepa mazima na pointi tatu kwenye mchezo wa Ligi Kuu England uliokuwa na ushindani mkuubwa. 

Baada ya dakika 90 kukamilika, ubao ulisoma Arsenal 0-3 Liverpool na kuwafanya mashabiki wa Arsenal kupoteza furaha yao.

Ni Diogo Jota ambaye alikuwa nyota wa mchezo kwa kuwatungua mabao mawili Arsenal inayonolewa na Mikel Arteta dakika ya 64 na 68.

Mohamed Salah raia wa Misri alicheka na nyavu dakika ya 68 na ulikuwa ni mchezo wake wa 150 kwenye Ligi Kuu England na bao lake la 93.

Liverpool ipo nafasi ya tano na pointi zao ni 49 huku Arsenal ikiwa nafasi ya 9 na pointi 42 na zote zimecheza jumla ya mechi 30.

Kinara ni manchester City akiwa na pointi zake 74 baada ya kucheza mechi 31.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic