April 6, 2021


 LUIS Miquissone, kiungo mshambuliaji wa Klabu ya Simba amesema kuwa kwenye mabao yake matatu ambayo amefunga ndani ya Ligi ya Mabingwa Afrika lile alilowatungua Al Ahly kwake ni moja ya bao bora kwa sasa.

Simba ikiwa imetinga hatua ya robo fainali baada ya kucheza mechi tano nyota huyo raia wa Msumbiji amefunga mabao matatu.

Bao la kwanza alifunga mbele ya Al Ahly wakati Simba ikishinda bao 1-0, bao la pili aliwatungua Al Merrikh, wakati Simba ikishinda mabao 3-0 na bao la tatu aliwatunga AS Vita, wakati ubao ukisoma Simba 3-0 AS Vita na yote alifunga Uwanja wa Mkapa.

Kiungo huyo ambaye ni miongoni mwa nyota waliokwea pipa leo kuelekea nchini Misri kwa ajili ya mchezo dhidi ya Al Ahly unaotarajiwa kuchezwa Aprili 9 amesema kuwa furaha yake ipo kwenye ushindi wa timu yake.

"Ninapenda kuona timu ikishinda na bao langu bora kwa sasa ni lile nililofunga dhidi ya Al Ahly," .

Bao hilo la Luis lilichaguliwa kuwa bao bora la wiki katika mashindano ya Ligi ya Mabingwa Afrika inayosimamiwa na Shirikisho la Soka Afrika, (Caf).

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic