April 19, 2021


 IMEELEZWA kuwa aliyekuwa kocha wa zamani wa kikosi cha Yanga, Mwinyi Zahara yupo kwenye hesabu za mwisho kuajiriwa ndani ya Simba ili akamilishe majukumu matano kwa kikosi hicho kinachonolewa na Kocha Mkuu Didier Gomes.

Zahera baada ya kuchimbishwa ndani ya Yanga aliweza kurejea tena ardhi ya Bongo ambapo alikuwa ni Mkurugenzi wa Benchi la Ufundi ndani ya Klabu ya Gwambina.

Habari zinaeleza kuwa miongoni mwa majukumu ambayo yatakuwa mikononi mwa Zahera ni pamoja na:-

Uvumbuzi wa vipaji vya wachezaji ndani ya ardhi ya Tanzania. Kuwaendeleza wale wenye ujuzi ili waweze kuwa bora na imara.

Mshauri kwenye masuala ya usajili wa wachezaji ikiwa ni wale wa ndani ya Tanzania pamoja na wachezaji wa kigeni.

Kujishughulisha na masuala ya mikakati ya timu.

Kushughulikia masuala ya kibiashara pamoja na masoko.

9 COMMENTS:

  1. Simba wanakosea huyu si muaminifu kwa simba

    ReplyDelete
  2. Hii sio sawa, achaneni na zahera tapeli huyo. Amekosa pa kwenda ndio aje aponee simba? No way hatumtaki ni agent wa utopolo huyo

    ReplyDelete
  3. Kama ni kweli utakuwa upumbavu wq hali ya.juu

    ReplyDelete
  4. Mpira hauopo hivyo nduguzanguni tuachaneni na mawazo ya kizamani professional ya mtu ibaki kuwa professional na mapenzi ya mtu kwa klabu yabaki Kama mapenzi tutamjaji kwa kazi mchawi mpe mtoto akulele

    ReplyDelete
    Replies
    1. Ujue kuna watu hawajui mpira, kisa Zahera aliifundisha Yanga basi hafai kufanya kazi simba. MBONA AJIBU KATOKA YANGA? GADIEL KATOKA YANGA? ZAHERA ANAUJUA MPIRA WA AFRIKA NA ANAJUA BIASHARA ZA MPIRA. YANGA WALISHINDWA WENYEWE TU PALE.

      Delete
  5. kuna wapuuzi wao wamekalili ujingaa
    .eti kisa zahera kawahi kufanya kazi Yanga basi hawamtaki aje Simba
    ndg soka la sasaa lipo kwenye uwezoo
    zahera kama vigezo vinamruhusu acha apige kazi Msimbazi

    ReplyDelete
  6. Mbona M/kiti wa yanga mzee Mshindo Msola alikuwa mchezaji wa Simba leo Mwenyekiti wa Yanga na wanakaribia kutwaa ubingwa?

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic