OLE Gunnar Solskjaer, Kocha Mkuu wa Manchester United amesema kuwa sababu kubwa iliyewapa ushindi mbele ya Granada ni nidhamu ya wachezaji pamoja na uwezo wa kutumia nafasi ambazo walizipata.
United ilishinda kwa mabao 2-0 dhidi ya Granada katika mchezo wa hatua ya robo fainali ya pili na kupenya mpaka nusu fainali kwa jumla ya mabao 4-0.
Ni Edinson Cavan dakika ya 6 alifungua pazia la mabao na Jesus Vallejo dakika ya 90 alijifunga na kuwafanya United kukata tiketi ya kutinga hatua ya nusu fainali ya Europa League wakiwa Uwanja wa Old Trafford.
Wanakwenda kukutana na Roma katika hatua ya nusu fainali ambayo ilishinda mbele ya Ajax kwa jumla ya mabao 3-2 baada ya robo fainali ya jana ubao wa Stadio Olimpico kusoma Roma 1-1 Ajax.
Ni Brian Brobbey dakika ya 49 alianza kufunga kwa Ajax na liliwekwa usawa na Edin Dzeko dakika ya 72 na kufanya ngoma iwe 1-1.
"Ndio naona tumeshinda na ninafurahi kwa sababu wachezaji walicheza kwa nidhamu na kujituma. Pia walipunguza makosa jambo ambalo limetupa furaha wote," .
0 COMMENTS:
Post a Comment