MOHAMED Abdalah, 'Bares', Kocha Mkuu wa Klabu ya JKT Tanzania amesema kuwa wachezaji wake wapo imara kwa ajili ya mchezo wa leo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Azam FC.
JKT Tanzania ipo nafasi ya 13 ikiwa na pointi 27 inakutana na Azam FC yenye pointi 47 baada ya kucheza mechi 25.
Bares amesema kuwa wanatambua ushindani ni mkubwa ila watapambana kupata pointi tatu mbele ya Azam FC.
"Tupo imara kwa ajili ya mchezo wa leo na kila mchezaji yupo tayari kuona kwamba tunapata matokeo hilo lipo wazi na tutaingia kwa kupata pointi tatu.
"Kikubwa ni kuona kwamba tunapata pointi tatu muhimu hivyo mashabiki watupe sapoti katika mchezo wetu wa leo," .
0 COMMENTS:
Post a Comment