April 13, 2021


MANCHESTER United inayonolewa na Kocha Mkuu, Ole Gunnar Solksjaer inaelezwa kuwa hawajakata tamaa kuhusu dili lao la kuihitaji saini ya winga wa Borussia Dortmund na nyota wa timu ya taifa ya England, Jadon Sancho. 

Mwaka uliopita, United walikuwa kwenye mstari wa mbele kuisaka saini ya winga huyo ila mwisho wa siku walifeli kumpata nyota huyo mwenye miaka 21 ambaye bado anashiriki Bundesliga kwa sasa.

Ripoti zimeeleza kuwa mabosi wa Manchester United jicho lao la kwanza kwenye dirisha la usajili ni kwa Sancho na wanahitaji kumuona akiwa katika Uwanja wa Old Trafford msimu ujao.

Mtendaji Mkuu wa Klabu ya Dortmund, Hans Joachim wiki iliyopita aliweka wazi kuwa klabu hiyo inajiandaa kumuuza Sancho kwa ofa nzuri ambayo itafika mezani.

"Bado siwezi kujihusisha kwenye masuala ya kufikirika, hilo sio jambo zuri lakini Jadon Sancho amekuwa bora muda wote ni sawa na Erling Haalad. Nimezungumza na Jadon pia kuhusu suala hilo.

"Ikiwa kutakuwa na ofa nzuri lazima tujadili suala hilo pamoja na wakala wa mchezaji," amesema.

Kwa msimu huu licha ya kusumbuliwa na majeraha, Sancho ametoa jumla ya pasi 16 za mabao kwenye mashindano yote.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic