April 13, 2021


KLABU ya Simba itawatambua wapinzani wake Aprili 30 baada ya Shirikisho la Soka Afrika kupanga ratiba za mechi zake baada ya kutinga hatua ya robo fainali.

Simba chini ya Didier Gomes imefanikiwa kutinga hatua hiyo baada ya kukusanya pointi 13 kwa msimu wa 2020/21.

Timu ambayo inaweza kukutana na Simba kwenye hatua ya robo fainali ni moja kati ya hizi hapa:-MC Alger na CR Belouizdad hizi zote ni za Algeria pamoja Kaizer Chiefs ya Afrika Kusini.

Kuhusu timu hizo Gomes amesema kuwa anatambua ubora wa wapinzani wake ila yeye hachagui wa kucheza naye.

"Natambua uimara wa timu ambazo ninaweza kukutana nazo lakini sina mashaka na hilo, nimewaambia wachezaji wanapaswa kujiamini ili kuendelea kusaka ushindi," .

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic