KOCHA Mkuu wa Simba Mfaransa Didier Gomes ametaja siri ya kiwango cha kipa wake namba moja Aishi Manula kuongezeka hivi sasa akiwa na timu ya taifa, Taifa Stars na klabu yake.
Hiyo ni
baada ya kuzua mijadala katika mitandao ya kijamii kutokana na kiwango hicho
pamoja na kumwagiwa sifa na Shirikisho la Soka Afrika (Caf) kupitia mitandao
yake ya kijamii.
Manula
ameweka rekodi ya kutoruhusu bao katika hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa
Afrika akiwa amecheza michezo mitatu kati ya minne ya makundi dhidi ya AS Vita,
Al Ahly na Al Merrekh.
Gomes amesema kocha wake mpya wa makipa Mbrazili Milton
Nienov ndiye aliyemuongezea ubora wa kuokoa michomo golini kwake.
Gomes
amesema kuwa tangu kocha huyo amejiunga na timu hiyo ameonekana akiwapa mbinu
tofauti za kuokoa hatari golini, ambazo leo hii zinamfanya Manula na makipa
wenzake Beno Kakolanya na Ally Salum kuonekana bora.
Aliongeza
kuwa kitu kingine alichoongezewa kipa huyo ni hali ya kujiamini akiwa golini
kwake na hiyo imemfanya ubora wake uongezeke zaidi.
“Manula
ni kati ya makipa bora niliowahi kukutana nao katika baadhi ya timu nilizopita
kuzifundisha, hivyo nina imani naye sana akiwepo golini.
“Wengi
wamekuwa wakihoji ubora wake kuongezeka, ukweli ni kwamba kocha mpya wa makipa
aliyejiunga na timu Milton ndiye anayefanya yeye aonekane bora katika kila
mchezo.
“Kwani
amekuwa akimpa mbinu mbalimbali zitakazomuwezesha kuokoa hatari golini kwake.
Pia amemuongezea hali ya kujiamini awapo golini kwake yeye pamoja na wenzake
Kakolanya na Ally,” alisema Gomes.
0 COMMENTS:
Post a Comment