April 4, 2021


 UONGOZI wa Simba umeweka wazi kwamba malengo yao kwa sasa ni kutinga hatua ya nusu fainali kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika.

Ikiwa na pointi 13 imeshakata tiketi ya kutinga hatua ya robo fainali kwa msimu wa 2020/21 na inaongoza kundi A ambalo lilikuwa linaonekana kuwa na vigongo vikali.

Imetinga pamoja na Al Ahly ya Misri ambayo ina pointi 8 na itakutana nayo Aprili 9, nchini Misri baada ya ule mchezo uliochezwa Uwanja wa Mkapa Simba kushinda bao 1-0.

Na bao la ushindi lilifungwa na Luis Miquissone akiwa nje ya 18 kwa pasi ya mshikaji wake Clatous Chama, wengi wanapenda kumuita mwamba wa Lusaka.

Al Merrikh na AS Vita ambazo zilikuwa zinapewa nafasi ya kutinga hatua ya robo fainali zenyewe safari yao imeishia hatua ya makundi.

AS Vita iliyokubali kichapo cha mabao 4-1 dhidi ya Simba ina pointi 4 na A l Merrikh ina pointi 2.

Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara amesema kuwa baada ya lengo la kwanza la kutinga hatua ya robo fainali kutimia sasa hesabu zao ni kuona timu inatinga hatua ya nusu fainali.

"Ilikuwa dhamira yetu kuona kwamba timu inatinga hatua ya robo fainali. Lengo la kwanza limetimia sasa tunafukuzia lengo al pili ambalo ni kutinga hatua ya nusu fainali.

"Imani yetu ni kwamba na hili linakwenda kutimia kisha baada ya hapa sasa ninaamini kutakuwa na jambo jingine ila kikubwa nguvu zetu sasa ni hatua ya nusu fainali," amesema.

2 COMMENTS:

  1. Mipango ikiwekwa vizuri na kila idara (wachezaji, benchi la ufundi, viongozi pamoja na mashabiki) ikitimiza majukumu yake ipasavyo, hapana shaka yoyote nusu fainali tutaingia na kutusua vile vile, Inshallah tuombe uzima

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic