NYOTA wawili wa Yanga kesho wanatarajiwa kukosekana kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Gwambina FC utakaochezwa Uwanja wa Mkapa.
Nyota hao ni pamoja na beki Yassin Mustapha pamoja na Mapinduzi Balama aambao hawa walikosekana pia kwenye mchezo dhidi ya Biashara United kutokana na kuwa ni majeruhi.
Licha ya kwamba maendeleo yao kwa sasa ni mazuri bado hawajatengamaa kuweza kurejea kwenye mechi za ushindani.
Yanga ikiwa nafasi ya kwanza na pointi zake 54 inakutana na Gwambina FC iliyo nafasi ya 12 na pointi zake ni 30.
0 COMMENTS:
Post a Comment