April 3, 2021


 HEMED Morocco, Kocha Mkuu wa Namungo FC amesema kuwa wapo tayari kwa ajili ya mchezo wao wa kesho wa Kombe la Shirikisho dhidi ya Nkana FC ya Zambia na wanahitaji pointi tatu.

Namungo ipo kundi D, imecheza mechi mbili na kupoteza zote, ilianza kupoteza mbele ya Raja Casablanca bao 1-0 ugenini na ikapoteza kwa kufungwa mabao 2-0 dhidi ya Pyramids, Uwanja wa Mkapa.

Inakutana na Nkana FC ambayo nayo haijakusanya pointi baada ya kupoteza mechi zake zote mbili kwenye makundi jambo ambalo litaongeza ugumu kwenye mchezo huo.

Akizungumza na Saleh Jembe, Morocco amesema  alikusanya makosa kwenye mechi zilizopita jambo ambalo litawafanya waingie uwanjani kwa namna nyingine.

 “Makosa kwenye mechi zetu ambazo zimepita yanatufanya tuingie kwa hesabu za tofauti kukutana na wapinzani wetu ambao tunawaheshimu ila kwa kuwa tupo nyumbani hatuna mashaka.

“Wachezaji wana morali kubwa na nimewaambia kwamba wanapaswa wajiamini kila kitu kinawezekana. Ushindi ambao tutapata ni muhimu kwa timu na Tanzania kiujumla,” amesema.

5 COMMENTS:

  1. Dah wanazihitaji point tatu zao wenyewe

    ReplyDelete
  2. Namungo vs Namungo!! Hamko makini kabisa au ndo yale ya darasa la saba wanatosha!!

    ReplyDelete
  3. Labda Nkana ni ikiwa kwao Zambia lakini wakija bongo nao wanaitwa Namungo

    ReplyDelete
  4. Ahahaha, kumbe Namungo FC ndio Nkana FC

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic