DENI la Yanga dhidi ya mshambuliaji wake wa zamani, Amissi Tambwe linazidi kupaa kutokana na kwamba halilipwi au halijalipwa kwa wakati.
Tambwe
anaidai Yanga takribani dola 21,000 (zaidi ya Sh 48,696,600), hii ni baada ya
kupeleka madai yake katika Mahakama ya Usuluhishi (CAS) na mwisho yakatoka
majibu kwamba zile fedha za usajili na baadhi yake ya fedha za mishahara na
gharama za kuendesha kesi, Yanga illipe.
Kwa mujibu
wa Tambwe mwenyewe, anaamini fedha hizo zitakuwa zimefikia dola 22,000 au zaidi
kwa kuwa muda umepita na Yanga bado hawajalitekeleza hilo.
Deni hilo
linaweza kuendelea kuwa kubwa kila kukicha hasa kama Yanga wataendelea
kuchelewa kulilipa kwa kuwa sheria ziko wazi. Kuna kipindi, Yanga itaingia
katika wakati mgumu kwani inaweza kuzuiwa kusajili.
Ukiangalia
Yanga ni ileile kweli lakini chanzo cha deni hilo kinaanzia nyuma lakini upande
mwingine viongozi walio madarakani wanahusika pia.
Kwa Yanga
kutoa fedha kama hizo zinazotakiwa kwa wakati huu, haliwezi kwua jambo jepesi.
Na huenda linaweza likawa jambo gumu zaidi kwa kuwa wadhamini wanaweza wakawa
hawahusiki sana maana wangependa kujihusisha na mambo wanayoona yanaipeleka
klabu hiyo mbele na si madeni ya nyuma.
Kuna mambo
mengi yanawakabiri kipindi hiki na wangependa kuona wanayakamilisha au
wanayafanya kwa ufasaha kwa kuwa presha inazidi kuwa kubwa kutokana na mwendo
wa wapinzani wao, mfano Simba na hata Azam FC.
Maana yake,
wanajikuta wamewekeza zaidi katika nguvu nyingi katika mwendo wao kipindi hiki
lakini wanashindwa kujua, mambo haya ya madeni yanaweza kuja kuwa tatizo kubwa
zaidi hapo baadaye.
Ugumu wake
ni kwamba kadiri muda unavyozidi kusonga mbele, ndivyo deni linazidi
kuongezeka. Litaendelea kuongezeka na kutengeneza hasara kubwa zaidi kwa kuwa
hata hapo awali, halikuwa kubwa hivi lakini baada ya kesi likapanda.
Maana yake,
baadaye kama linazidi kuongezeka, Yanga itajikuta inalipa hadi dola 30,000 au
zaidi. Na utaona, hata kabla ya kesi, kulikuwa na hali ya kulipuuzia jambo hilo
hadi ilipofikia kesi kwisha.
Sasa Yanga
wasiendelee kurudia kosa linalofanana na lililowafanya wao kuingia kwenye
hasara hii. Badala yake, wamlipe Tambwe fedha zake lakini ikiwezekana kufanya
mawawasiliano ya kibinadamu dhidi ya wengine wanaowadai.
Kuwa salama,
Yanga lazima wajitahidi kumlipa Tambwe, lazima wakubali kuzungumza na wengine
ambao wanawadai na kuangalia njia sahihi na bora kuhakikisha wanalipa madeni
yao hasa ya wachezaji ambao waliachana nao.
Baada ya
kufanya hivyo, Yanga watakuwa na nafasi ya kufungua ukurasa mpya na baada ya
hapo wataendesha mambo yao kitaalamu na weledi zaidi na kuepukana na kesi kama
hizi ambazo wakati mwingine zitakuwa zinawatoa njiani bila ya sababu za msingi.
Nasema
inawatoa njiani kwa kuwa wanajikuta wanaanza kupambana na deni wakati huu si
wakati mwafaka kwao kuanza kufikira namna ya kulipa deni badala ya kufikiria
njia sahihi za kuisaidia timu kupambana na mwisho kupata mafanikio makubwa.
Wakati
fulani, wachezaji wa kigeni na hata wa hapa nyumbani walikuwa wakilalama
kudhulumiwa fedha zao na klabu mbalimbali lakini na hasa hizi kubwa na hakukuwa
na kesi nyingi.
Wakati huu
unaona watu wamebadilika, wachezaji wa kigeni ndio usiseme, watu wanajitambua
na wanajua njia zipi za kudai haki zao.
Badala ya
wale wanaodai haki zao kuchukuliwa kama maadui, badala yake klabu zijifunze na
kuliepuka jambo hili maana wachezaji kama unazungumza nao vizuri na ikiwezekana
wakaanza kulipwa taratibu, nao ni wanadamu lazima watakuwa waelewa na mwisho
mnamaliza salama.
Tunakarabati jengo kwanza
ReplyDeleteMlipe muajiriwa ajira yake kabla ya kukauka jasho lake. Kukopa ni harusi na kulipa ni matanga
ReplyDeleteHivi huna habari zaidi ya hizi za yanga
ReplyDelete