April 25, 2021

 


SHECKY Mngazija daktari wa Klabu ya Yanga amesema kuwa maendeleo ya wachezaji wa timu hiyo kwa sasa wanaendelea vizuri huku wengine wakiwa wameanza mazoezi.

Akizungumza kuhusu hali zao Mngazija amesema:" Kuhusu wachezaji ambao walikuwa na majeraha hali zao kwa sasa ni nzuri, ukianza na Mapinduzi Balama yeye inajulikana kwamba ana maumivu ya muda mrefu alipata matibabu Afrika Kusini na anaendelea vizuri ameanza mazoezi ya kutembea.

"Yassin Mustapha alipata maumivu ya nyama ya paja alipokuwa na timu ya taifa ameendelea kupata matibabu kwa kina na kwa sasa naye anaendelea vizuri.

"Feisal Salum aliumia siku moja kabla ya mechi dhidi ya Biashara, tayari ameanza mazoezi. Tuisila Kisinda alipata maumivu ya bega la kushoto naye pia anaendelea vizuri, " amesema.

Wachezaji hao leo kuna hatihati wakaukosa mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Azam FC, Uwanja wa Mkapa isipokuwa Fei Toto ambaye ameanza mazoezi na wenzake.

Pia nyota mwingine ambaye anasumbuliwa na majeraha ni Dickson Job ambaye yeye aliumia pia nyama ya paja naye anaendelea vizuri.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic