April 5, 2021

 


NYOTA wawili wa kikosi cha Yanga kilicho chini ya Kaimu Kocha Mkuu, Juma Mwambusi wamevuruga mipango ya kocha huyo kutokana na hali zao kutokuwa sawa kwa ajili ya mazoezi.

Yanga inaendelea na mazoezi katika kambi yao iliyopo Kigamboni kwenye kijiji cha Avic ikiwa ni kwa ajili ya maandalizi ya mechi za Ligi Kuu Bara pamoja na Kombe la Shirikisho

Mchezo wake wa kwanza baada ya ligi kurejea kwa kuwa ilisimama kutokana na maombolezo ya aiyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, John Pombe Magufuli, inatarajiwa kumenyana na KMC Uwanja wa Mkapa ambapo ni mchezo wa ligi wakiwa na kumbukumbu ya kupata ushindi wa mabao 2-1 kwenye mchezo wa kwanza uliochezwa Uwanja wa CCM Kirumba.

Kwa mujibu wa Ofisa Habari wa Yanga, Hassan Bumbuli amesema kuwa nyota wawili ambao walikuwa kwenye mpango wa kocha ni pamoja na Michael Sarpong pamoja na Balama Mapinduzi ila hawajawa fiti.

"Kikosi kipo sawa isipokuwa Balama Mapinduzi na Michael Sarpong hawa kwa pamoja wanaumwa.

"Kocha alitaka kutumia maandalizi haya kuwanoa vilivyo ili Sarpong aje kuwa lulu katika safu hiyo lakini kilichotokea imemfanya kujisikia vibaya," .

Yanga ipo nafasi ya kwanza kwenye ligi ikiwa na pointi 50 baada ya kucheza jumla ya mechi 23.

Chanzo:Spoti Xtra

6 COMMENTS:

  1. Jamani tuwe serious kidogo basi, nyota wawili ndio wanavuruga mipango mizima ya kocha?

    ReplyDelete
  2. Utopolo bhana, balama mwenyewe haha mechi hata moja ndo kaanza mazoezi juzi tu leo anavuruga mipango.... Msitafute visingizio

    ReplyDelete
  3. Kocha wetu usihofu we peleka timu tu hata tukifungwa hatutakulaumu kwani tunajua kuwa hatuna timu

    ReplyDelete
  4. Tunacho kikosi kipaana kama kile cha watani kama vile vile Bocco wa mstsari wa mbele hayupo kikosini na ndio hivo hivo hapana kitachoharibika

    ReplyDelete
  5. Mimi nawashauri watani zangu Utopolo waendelee kuijenga timu yao kwa ajili ya kushiriki ligi ya mabingwa Africa kwa sababu tayari Mnyama amekwisha wabeba mgongoni hivo msipoteze muda kulilia ubingwa wa ligi kuu Tanzania Bara ambao hawataupata. Ni ushauri tu... 😂😂😂

    ReplyDelete
    Replies
    1. Shida nafasi ya pili na ya 3 wakikosa hawaendi

      Delete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic