April 5, 2021

 


MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Wydad Casablanca ya Morocco, Mtanzania, Simon Msuva amefichua kuwa ndoto zake msimu huu ni kuhakikisha anakuwa mfungaji bora kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Msuva mpaka sasa ameshafunga mabao mawili katika hatua ya makundi ya michuano hiyo na timu yake ipo kundi C.

 

 Msuva amesema kuwa malengo yao katika michuano hiyo ni kuchukua ubingwa pamoja na kuwa mfungaji bora kutokana na kuanza vizuri.


“Kwanza Wydad ni timu kubwa ambayo itanifanya nionekane zaidi na tunashiriki michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika, malengo yetu ni kuchukua ubingwa wa Afrika lakini pia ubingwa wa Morocco.

 

“Lakini nashukuru nimeweza kuanza vizuri na tayari nimeshafunga mabao mawili katika hatua ya makundi na sasa matumaini yangu ni kuendelea kupambana ili ikiwezekana niwe mfungaji bora wa michuao hii ambayo itaongeza kitu kwenye wasifu ‘CV’ wangu,” amesema Msuva.

5 COMMENTS:

  1. Msuva pambana tu ndugu lakini ujue huku kwetu Tanzania kuna vijana wanakiwasha aiseee,kwahiyo unatakiwa kujipanga MZEE.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Da ume mwambia ukwel kna chamana luis ni atal ana mawil 2 wakat wenzie wana 3

      Delete
  2. Kwa kwel kaka msuva hiyo nafasi ni ngumu Ila matumaini ni bora

    ReplyDelete
  3. Pambana bro hata Mimi naamin hvoo

    ReplyDelete
  4. Pambana wewe ndio bendela yetu,tunakuombea

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic