April 2, 2021

 


SELEMAN Matola, Kocha Msaidizi wa Klabu ya Simba amesema kuwa kesho wanahitaji kupata matokeo chanya mbele ya AS Vita.


Simba itawakaribisha AS Vita Uwanja wa Mkapa kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika hatua ya makundi ukiwa ni mchezo wa tano.


Mchezo wa kwanza walipokutana DR Congo,  ubao ulisoma AS Vita 0-1 Simba na bao lilipachikwa na Chris Mugalu kwa mkwaju wa penalti. 


Matola amesema:"Tunahitaji ushindi katika mchezo wetu wa kesho tunatambua ushindani utakuwa mkubwa ila tupo tayari.

Ameongeza kuwa wachezaji wote wapo fiti na hakuna ambaye watamkosa kwa sababu wale ambao walikuwa na majukumu katika timu zao za taifa wamerejea.


Miongoni mwa wachezaji waliokuwa na timu zao za taifa ni pamoja na Luis Miquissone raia wa Msumbiji, Clatous Chama raia wa Zambia, Meddie Kagere wa Rwanda, Mohamed Hussein, Shomari Kapombe, Aishi Manula walikuwa na timu ya Taifa ya Tanzania.


Kwenye kundi A Simba ina pointi 10 ikiwa nafasi ya kwanza na AS Vita ipo nafasi ya tatu na pointi 4 zote zinahitaji ushindi ili kufikia malengo ya kutinga robo fainali.

Simba inahitaji pointi moja kujihakikishia nafasi ya kutinga robo fainali huku AS Vita wakihitaji pointi tatu kufufua matumaini ya kutinga hatua ya robo fainali hivyo hautakuwa mchezo mwepesi.


7 COMMENTS:

  1. Kila la kheri mnyama. Kesho ni kufa na kupona Vita afe

    ReplyDelete
    Replies
    1. Hii mechi ni zaidi ya Do or die season two.Hii Ni Dying fighting for something to the end.Ndani ya akili ya wachezaji wa Vita mawazo yao ni hayo tu, kuja kwa mkapa na kuondoka na point tatu za Damu na wanajua haitokuwa rahisi ya hivyo lakini unaona kabisa moral ya wachezaji vita ipo tayari kwa Vita kuu.Simba na hasa wachezaji wanatakiwa kuwa zaidi ya kuwa makini wanatakiwa kujitoa kwenye mechi ya kesho la sivyo wataliingiza Taifa kwenye msiba mwengine wakati watanzania wengi wanahitaji kitu Cha kupunguza makali ya uchungu ya msiba wa Taifa ya kuondokewa na Raisi kipenzi Cha Tanzania na Africa Muheshimiwa Magufuli.

      Delete
  2. Kufungwa sio rahisi labda wapate suluhu.

    ReplyDelete
  3. Dilunga, Morrison, mugalu, beki line wawepo walewale, team onyango, hakuna atakaepita.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic